KAMSHINA MMOJA AONDOLEWA KWENYE LIGI
Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana
(Septemba 25 mwaka huu) kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya
Vodacom ambazo zimeshachezwa mpaka sasa, na kuzifanyia uamuzi wa
kikanuni ikiwemo kumuondoa Kamishna mmoja.
George
Komba aliyekuwa Kamishna kwenye mechi namba 20 kati ya Simba na Ruvu
Shooting ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi kutokana na
upungufu uliojitokeza katika ripoti yake.
Klabu
ambazo zimeandikwa barua za onyo ni African Lyon kwa kwenda uwanjani na
jezi tofauti na zile ilizoonesha kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi
(pre match meeting), Mtibwa Sugar kwa kuchelewa kuwasilisha leseni za
wachezaji wake wakati wa mechi na Ruvu Shooting kwa ushangiliaji
uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya Simba.
Kamati
pia imethibitisha kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko
Kessy Mapande wa JKT Ruvu, hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1)() anakosa
mechi tatu na kulipa faini ya sh. 500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi
namba 20, 27 na 80.
Kwa
upande wa waamuzi, Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na
upungufu alioonesha kwenye mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wamiliki
wa viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya
wameandikiwa barua ya kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo
mbalimbali yenye upungufu ikiwemo uzio wa kutenganisha wachezaji na
washabiki.
Mchezaji
Faustin Lukoo wa Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi
aliyemtoa nje kwa kadi nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye
mechi dhidi ya African Lyon na Katibu wa Oljoro JKT aliyemwaga maji
kwenye chumba cha timu ya Polisi Moro, masuala yao ni ya kinidhamu,
hivyo yamepelekwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kwa ajili ya hatua
zaidi.
Kwa
klabu ambazo timu zao mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya
mdhamini, suala hilo limepelekwa kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe
ndiyo wanaogawa vifaa hivyo.
0 comments:
Post a Comment