Sunday, September 30, 2012

BONDIA FRANCIS CHEKA AMTWANGA KARAMA NYILAWILA KWA KO RAUNDI YA 6

BONDIA Francis Cheka jana usiku alimpiga kwa KO bondia Karama Nyilawila kwenye pambano la raundi 12 la UBO

Cheka alimpiga Nyilawila kwa KO raundi ya sita alipomtwanga ngumi iliyompeleka chini na kumfanya refa kumwesabia lakini aliponyanyuka aliamua kuvua gloves kuahashiria amekubali matokeo.

Cheka ambaye aliingia ulingoni bila mbwembwe alimwacha Nyilawila ajifurahishe kwa kurusha makonde ambayo alikuwa anayakwepa hivyo kumfanya pumzi kumwishia mapema.

Ilipotimu raundi ya tano Cheka alianza kurusha ngumi nzito nzito na kufanya ukumbi kulipuka kwa kelele za kusema " Cheka ua huyo unampotezea muda, maliza"

Bondia Karama Nyilawila akiwa amekaa ulingoni baada ya kupokea konde lililompeleka chini wakati wa pambano la UBO lililofanyika jana usiku ukumbi wa PTA sabasaba.

Bondia Francis Cheka akipangua ngumi aliyorusha Karama Nyilawila

Bondia Karama Nyilawila akiwa amemkumbatia Francis Cheka

0 comments: