Monday, September 17, 2012

MASHINDANO YA NGUMI ZA RIDHAA NGAZI YA TAIFA ZAANZA LEO UWANJA WA NDANI WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Bondia Said Hofu aliyevaa red akipigana na Emanuel Mogella wa Ilala kwenye mchezo wa kg 49 uliochezwa leo jioni na bondia Said Hofu alishinda baada ya mwamuzi kukatisha pambano kumnusuru Emanuel Mogella kwani alizidiwa sana.

Bondia Joseph Meshack wa Arusha aliyevalia red akipigana na bondia Fadhili Hassan wa Pwani aliyevaa blue  kwenye mchezo  uliochezwa uwanja wa Taifa wa ndani leo jioni, Joseph Meshack alishinda kwa pointi  



MASHINDANO ya ngumi za ridhaa yameanza leo jioni kwa mabondia wa uzani wa kg49, kg 52 na kg 64 kupanda ulingoni.
Jumla ya michezo 12 imechezwa leo na inatarajwa kuendelea tena kesho asubuhi kuanzia saa 4 asubuhi kabla ya kufunguliwa majira ya saa 9 alasiri na mwenyekiti wa baraza la michezo Dioniz Malinzi.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu, Makore Mashaga amesema mashindano ya mwaka huu yanaonekana yana msisimko mkubwa kuliko miaka ya nyuma ila tatizo ni ukata tu unawakabili.

0 comments: