Mkurugenzi wa LINO Agency akiongea na waandishi wa habari |
Mashindano
ya Redds Miss Tanzania yamekamilika katika hatua zote na hatua ya
mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo nayo imekamilika na kufanikiwa
kuwapata warembo jumla ya 30.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla
katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa
fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia
90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine
wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika
shindano la mwaka huu.
Baada ya kukamilika kwa mashindano hayo ya
Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia
katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya
jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kitalii ya GIRAFFE
HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa
kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda kuwajulisha wadau wa tasnia ya
urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi
tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).
Kwa Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds
Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania
wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia
ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa kuingia
hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa
kuzingatia mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa
Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa
kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao.
2013.
0 comments:
Post a Comment