Friday, September 7, 2012

ZUBERI UBWA AOMBEWA ICT

BEKI aliyetupiwa virago na Yanga msimu uliopita, Abuu Zuberi Ubwa mwenye umri wa miaka 20, ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Shirikisho la Soka Ureno (FPF) ili acheze soka ya kulipwa huko.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura aliwaambia waandhishi wa Habari jana mbali na Ubwa, ambaye ni alikuwa beki wa kushoto Yanga, kwa misimu miwili ya kuwa na klabu hiyo,mwingine ni Hamisi Thabit Mohamed mwenye umri wa miaka 19 kutoka African Lyon pia ameombewa ITC ya kucheza nchi hiyo.

Kwa mujibu wa FPF, wote wawili wanaoombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa (amateur) ili waweze kujiunga na timu ya Atletico Sport Clube ya Ureno ambayo hata hivyo haikuelezwa iko daraja gani nchini humo.

Pia FPF imeombwa kupatiwa hati ya maelezo ya mchezaji (player’s passport) kwa kila mmoja ikiwemo taarifa za ushiriki wao katika mechi rasmi zinazotambuliwa na TFF wakiwa katika klabu zao hizo za zamani.

Wachezaji Zuberi Ubwa na Hamisi Mohamed wanafanya idadi ya wachezaji ambao hawana timu walioombewa ICT kufikia tatu baada ya ile ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB)  kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili aweze  kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.

0 comments: