Mwili wa
aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness Christopher Yamo
umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa safari ya mazishi kesho
mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New Habari 2006 Limited, alifariki
dunia jana katika hospitali ya Jeshi, Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa
kwa matibabu.
Katika uagwaji
wa mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi, mamia walijitokeza
na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa
huzuni, simanzi na majonzi eneo la tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke
pema peponi roho ya marehemu, Amin. Picha na habari kwa hisani ya Mtandao wa Bongostaz.blogspot.com
Waombolezaji |
Waombolezaji |
Mdau BinZuber (kulia) akiwa na mdau mwingine walikuwa ni mmoja wa watu walifika kumuada dada yetu kipenzi Agnes.
mama akibembelezwa ilihsuzunisha sana!.
Mama huyu alishindwa kujizua akipatiwa msaada.
Vilio vilio vilio, hakika Agnes tulikupenda ingawa Mungu alikupenda zaidi.
inasikitisha ni vilio kila kona!.
Huzuni! huzuni!
katika ibada ya Agnes
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda |
Mkurugenzi wa Tanzania Daima, Lillian Mbowe |
Huyu alishindwa kujizuia aliishiwa nguvu hapa anapata msaada.
Mamaa pipiro mdau wa spotlady blog akiwe kwenye tafakuro kubwa.
Waombolezaji, Asha Bani kushoto Ratifa Baranyikwa kulia pamoja na mdau mwingine (katikati) wakiwa na huzuni kubwa baada ya kuondokewa na mfanyakazi mwenzao Agnes.
Mwili wa Agne ukipandishwa kwenye gari tayari kwa safari mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
0 comments:
Post a Comment