Thursday, September 27, 2012

RAMBIRAMBI MSIBA WA ERASTO ZAMBI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea jana Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi.

 
Zambi ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili Septemba 30 mwaka huu kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.
 
Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.
 
TFF inatoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Zambi mahali pema peponi. Amina
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments: